Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Hawzah Imam Ridha (a.s) iliyopo chini ya Taasisi ya "Hojjatul Asr Society of Tanzania", Ikwiriri - Tanzania, inayoongozwa na Maulana Samahat Sayyid Arif Naqavi (H.A) inaendelea na harakati zake za kielimu katika madarasa mbalimbali ya Hawzah hii. Maulana Samahat Sayyid Arif Naqavi, Kiongozi Mkuu wa Taasisi hii, amefanya ziara muhimu katika vituo mbalimbali vya Kidini vya Taasisi hii ikiwe Hawzah hii ya Imam Ridha (a.s). Elimu ni Nuru, na Ujahili ni Giza.

14 Aprili 2025 - 15:43

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) azidi kuiweka na kuithabitisha Elimu hii ambayo ni Nuru katika nyoyo za Wanafunzi hao, na azidi kuwapa Taufiq, swiha na afya njema Viongozi, Walimu, na Wasimamizi wa Taasisi hii na Hawzah zote zilizopo chini yake, ili ziendelea kueneza na kusambaza nuru ya elimu na maarifa na kuondosha giza katika jamii za waja wa Mwenyezi Mungu nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Habari Pichani | Harakati za Kielimu za Hawzat Imam Ridha (a.s) iliyopo chini ya Taasisi ya "Hojjatul Asr Society of Tanzania" -Ikwiriri- Tanzania

Your Comment

You are replying to: .
captcha